welcome

finally you made it in!!!!!!!!!!

Matatizo Lyrics By Harmonize

Matatizo lyrics – Harmonize
Source Victor Matara

(verse One)

Aiee ma, olelelele
alfajiri imefika, anga inang’aa
mvua inaanza katika,
ghafla tumbo la njaa,
naweka sauti kwa spika
nipate umbea wa dar
mara simu inaita
jina la anko twah akisema,
mama yu hoi kitandani,
mama si wa leo wa kesho
na kupona sizani upate japo neno la mwisho

(Bridge)
Mi ndo mtoto wa pekee
nyumbani wananitegemea,
mdogo wangu wa kike aliduni alishaga olewa
tizama jasho langu la mnyonge,
kipato hakikidhi mahitaji,
napiga moyo konde,
Yarabi mola ndio mpaji

(Chorus)
Matatizo, yatakwisha lini
Matatizo, kila siku mimi
Matatizo, yatakwisha lini
Japo likizo nifurahi na mimi.

(verse two)

mola aliniumba na subira ,
imani pekee ngao yangu,
mbona nishasali sana ,
ila bado tafarani,
mama kanifunza kikabira,
ikunde sanda haimi yangu,
tena nijitume sana,
na vya watu nisivitamani
ata mpenzi nilonaye,
najua siku atanikimbia,
itanitesa ye ndio nguzo oh
zile ngoja kesho baadaye,
atachoka kuzivumilia,
anakosa ata matunzo -oh,
ona aa,nadaiwa kodi nilipopanga ,
nashinda rodi nikiranda,
nishapiga hodi kwa waganga,
kwa kuhisi narogwa,
nikauza maji na karanga,
nikawa dobi kwa viwanda,
ila kote ziro ni majanga,
mtindo mmoja,

( chorus)

Get More Juicy News